Kwa mujibu wa ripoti ya kitengi cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, kamati za wanawake wa Hezbollah, kwa msaada wa Ali Al-Miqdad, mbunge kutoka Kundi la Uaminifu kwa Muqawama, ziliandaa maonyesho na semina yenye kichwa cha habari kisemacho: “Umbusho wa Mashahidi” katika makaburi ya mashahidi wa Brital kwa anuani ya “Kuhudhuria kwenye Ukumbusho” kwa kushirikiana na kundi la wasanii wanawake wa sanaa ya maonyesho pamoja na watu wa siasa, dini na jamii.
Maonyesho haya yalihusisha vitu binafsi na nguo za mashahidi, pamoja na kazi za sanaa zilizoonyesha dhana ya kujitolea na sadaka ya nafsi.
Al-Miqdad katika hafla hiyo alisema: “Shahidi ni mfano wa juu wa kujitolea, mashahidi wametupa nguvu na heshima, na tunapaswa kuilinda damu na dhamira yao.”
Alisisitiza kuwa: “Silaha za Muqawama hazitawasilishwa, zina idhamini Lebanon dhidi ya maadui wa Kizayuni, na jitihada zote za kudhoofisha nafasi yake zitaanguka.”
Mwenyekiti wa Kundi la Muqawama alirejelea kusena: “Imam Musa Sadr, wakati Lebanon ilikuwa bila serikali au jeshi na ikivamiwa, alianza njia ya mashahidi kutoka ‘Ain al-Baniyah’, Muqawama ulikuwa ni hitaji la kihistoria kwa ajili ya kulinda taifa.”
Aliongeza kuwa: “Ardhi yetu ni Karbala, na Muqawama utaendelea hadi pale uvamizi utakapokoma, Kila mtu anayejua kusalimisha silaha zake atapoteza heshima na utu wake.”
Al-Miqdad kwa niaba ya “washirika wa ndani” alisema: “Fikiria kuondoa hoja ya kuwasilisha silaha kutoka akilini mwenu, na anza kwa kuwatimua Wazayuni kutoka katika ardhi yetu iliyokaliwa na kuachiliwa wafungwa wetu, baada ya hapo, tunaweza kujadili suala hili.”
Alisisitiza kuwa: “Jeshi la Lebanon lina heshima kubwa, lakini limezuiliwa kutumia silaha za kisasa kwa ajili ya kulinda nchi.”
Al-Miqdad alimalizia kwa kusema: “Ghaza leo inakabiliwa na njaa, na zaidi ya mashahidi 60,000 wameuawa pale chini ya dhana ya msaada wa kimataifa, wakati Lebanon bado iko hatarini na adui hajataka kutoka kwenye ardhi yetu iliyokaliwa na anaendelea na uvamizi wake.”
Maoni yako